KIPATO KIKUBWA KISICHOTARAJIWA HUWACHANGANYA WASANII, ASEMA CRAZY GK



KIPATO KIKUBWA KISICHOTARAJIWA HUWACHANGANYA WASANII, ASEMA CRAZY GK
KIPATO KIKUBWA KISICHOTARAJIWA HUWACHANGANYA WASANII,            ASEMA CRAZY GK

Mkali wa long time kwenye muziki wa kizazi kipya Gwamaka Kaihula maarufu kama Crazy GK amesema moja ya vitu vinavyowachanganya wasanii ni kupokea kipato kikubwa kuliko walivyotarajia.

Akizungumza na EFM Radio kupitia kipindi cha Genge wakati akitambulisha ngoma yake mpya "Shukran", GK akasema mara nyingi maisha ya wasanii yanabadilika na wakati mwingine kuingia kwenye makundi mabaya kutokana na mafanikio ambayo hawakuyatarajia na hali huwa mbaya zaidi pale mafanikio yake ya ghalfa yanapotoweka.

"Sisi wasanii wengi tunatokea kwanye maisha ya hali ya chini na pengine tulikuwa hatutarajii makubwa sana. Unapiga hesabu za kupata laki moja lakini badala yake unapata milioni tano, ni lazima uchanganyikiwe," alisema GK.

Mkali huyo wa kundi lililotamba sana East Coast Team (ECT) alisema inahitaji utulivu wa hali ya juu kwa msanii ili kulinda heshima yake na kuepuka kujiingiza kwenye makundi mabaya yakiwemo ya utumiaji madawa ya kulevya.



Comments