Khedira kuondoka Real Madrid


Khedira kuondoka Real Madrid

757872_heroaNa Augustino Mabalwe,Dar es salaam

Baada ya kukosa namba kwa muda mrefu katika kikosi cha Carlo Ancelotti,kiungo Sami Khedira amethibitisha kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika klabu hapo.

Khedira,27, ambaye ameichezea timu hiyo zaidi ya mechi 100 tangu ajiunge na matajiri hao miaka mitano iliyopita,sasa amepoteza nafasi ya kucheza kufuatia uwepo wa Luka Modric na Tony Kroos aliyesajiliwa msimu huu akitokea Bayern Munich. "Bado sijafanya mazungumzo na klabu yoyote na sijasema nitaenda timu gani.Kwa sasa bado naitumikia Real Madrid lakini baada msimu huu nitatafuta sehemu ya kuendeleza soka langu " alisema Khedira

Mkataba wa kiungo huyo katika klabu ya Real Madrid unamalizika mwishoni mwa msimu huu na timu hiyo imeonekana kugoma kuanzisha mazungumzo juu ya mkataba mpya na mjerumani huyo.

Klabu za Schalke 04, Chelsea, Arsenal na Bayern Munich zinapigana vikumbo kuwania saini ya kiungo huyo.



Comments