JUVENTUS YAIFUMUA BORUSSIA DORTMUND NYUMBANI 3-0 LIGI YA MABINGWA, YASONGA MBELE KWA BAO 5-1 …Carlos Tevez noma
Miamba ya Italia Juventus imeingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kibabe baada ya kuifumua Borussia Dortmund 3-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani Signal Iduna Park.
Katika mchezo wa kwanza Borussia Dortmund wakachezea kichapo cha bao 2-1 ugenini na hivyo kuaga michuano kwa jumla ya bao 5-1.
Magoli ya Juventus yalifungwa na Carlos Tevez aliyetupia mawili dakika ya 3 na 79 huku bao lingine likiwekwa wavuni na Alvaro Morata dakika ya 79.
Comments
Post a Comment