Mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic amesema wachezaji wa Chelsea walijifanya kama watoto katika matukio kadhaa na kupelekea yeye kulimwa kadi nyekundu ya utata katika mchezo wa wa Ligi ya Mabingwa uliofanyika Jumatano usiku.
Raia huyo wa Sweden alitolewa baada ya kumchezea visivyo kiungo wa kati wa Chelsea Oscar kunako dakika ya 31 lakini PSG ikafanikiwa kuizuia Chelsea na hatimaye kufuzu kwenda hatua ya robo fainali.
"Nilipopewa kadi nyekundu wachezaji wote wa Chelsea walinikaribia na kunizunguka," anaeleza Zlatan Ibrahimovic.
''Sijui nikasirike ama kucheka. kwangu mimi wakati nilipoona kadi nyekundu nilijisemea kuwa refa huyu hajui anachofanya'', anaongeza mchezaji huo wa PSG.
Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 33, pia alisema kwamba Oscar alijidai kuumia baada ya tukio hilo. "Sijui iwapo alikuwa anajifanyisha ama vipi, kitu muhimu ni kwamba tuliibuka washindi''.
Mechi hiyo iliochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge ilikamilika ikiwa 2-2 na kuunda jumla ya mabao 3-3 kwa michezo yote miwili huku PSG ikifuzu kwa kupata mabao mengi ya ugenini.
Comments
Post a Comment