Huyu ndio muasisi wa matumizi kadi katika Kombe la Dunia


Huyu ndio muasisi wa matumizi kadi katika Kombe la Dunia

8665083eb7b6ed64b483488697cdb288Na Amplifaya

KEN ASTON hili si jina linalofahamika sana miongoni mwa mashabikiwa mpira wa miguu duniani lakini katika vitabu vya FIFA jina hili liko ukurasa wa mbele kabisa kuliko jina la raisi wa
sasa wa FIFA Sepp Blatter.

Je Ken ni nani hata aheshimike namna hii?

Alikuwa ni mwamuzi wa Kiingereza aliyekuja na wazo la matumizi ya kadi za njano na nyekundu kwenye mchezo wa soka.

Akisimulia jinsi alivyoupata msukumo huo Ken anasema `ilikuwa ni katika kombe la dunia la mwaka 1966 nchini England kwenye mchezo Wa robo fainali kat ya Argentina na England nilimuona mwamuzi mwenzangu Rudolf Keitlin (huyu alikuwa ni Mjerumani) akipata wakati mgumu kumtoa nje ya uwanja mshambuliaji wa
Argentina, Antonio Rattin aliyekuwa amefanya madhambi dhidi ya mchezaji wa England"

Mwamuzi Rudolf hakuwa akijua Kiagrentna hivyo hivyo Rattin hakujua Kijerumani basi ikawa ni kituko pale uwanjani kifupi hakukuwa na maelewano.WCUP WORLD CUP SOCCER ITALY FRANCE FINAL

Hapa ndipo nilipopata wazo la kuwa na ishara ambayo itakuwa wazi na yenye kufahamika kwa wote ili kuondoa usumbufu kama alioupata bwana Rudolf siku ile (Nilitazama pia kazi za taa za
kuongozea magari barabarani kwamba njano jiandae na nyekundu Ondoka) baada ya wazo langu kukubalika tulizitumia kadi
hizo kwa majaribio katika michuano ya soka ya Olympic ya mwaka 1968.

Miaka miwili baadae yaani mwaka 1970 ndipo yalipoanza matumizi ya kadi hizo kwa Mara ya kwanza katuka kombe la dunia lililofanyka huko Mexico, huku mwaka 1982 ikawa rasmi kwa ligi zote duniani" anasema Ken.Ronaldo-Howard-Webb-004

Fainali yenye kadi nyingi zaidi nyekundu ni ya mwaka 2006 (Ujerumani ) ambapo kadi 30 nyekundu zilitolewa, 23 Ufaransa mwaka 1998, Korea Kusini na Japan, 2002 wakifungana nafasi
ya na fainali za 2010 Afrika Kusini kwa kutoa kadi 17 kila moja.

Huku mchezo unaoshikilia rekodi ya kuwa na kadi nyingi nyekundu ni kati ya Ureno na Uholanzi (2006) ambapo kadi nne nyekundu zilitolewa , na16 za njano zikitolewa katika mchezo huo.

Je nani anashikilia rekodi ya kadi nyekundu ya mapema zaidi katika historia ya kombe la dunia?jose-batista

Ni Jose Batista wa Uruguay katika fainali za mwaka 1986 alipewa kadi sekunde ya 56 ya mchezo baada ya kumkwatua kwa nyuma mchezaji wa Scotland, Gordon Strachan.



Comments