Ni dhahiri sasa Theo Walcott anataka kuufikia mshahara wa Mesut Ozil baada ya kuitaka klabu yake ya Arsenal kumwongezea mshahara zaidi kwa wiki.
Awali mshambuliaji huyo alikua akipokea kitita cha pauni 90,000 lakini sasa ameitaka klabu yake hiyo imlipe pauni 100,000 ambazo ni sawa na zaidi ya milioni 260 ndani ya wiki moja akitofautiana kidogo na Ozil ambaye analipwa pauni 140,000.
Theo Walcott ambaye amerejea hivi karibuni, sasa anaitaka Arsenal kumuongezea mshahara hadi kufikia pauni 100,000 (Sh milioni 260) kwa wiki.
Walcott alikuwa majeruhi kwa kipindi kirefu lakini amerejea na kuanza kuonyesha kiwango kizuri.
Comments
Post a Comment