Hatima ya Ngassa bado haijajulikana Yanga



Hatima ya Ngassa bado haijajulikana Yanga

ngassa-goalNa George Mganga "Amplifaya"

Yanga imetamka kuwa haina lengo la moja kwa
moja kuachana na mshambuliaji wao Mrisho
Ngassa na katika kuthibitisha hilo kwa vitendo,
tayari uongozi wa klabu hiyo umeweka mezani
Sh. 80 Milioni wakimtaka asaini dili jipya la
kumbakisha timu hiyo.

Mmoja wa mabosi wa klabu hiyo aliyeko katika
kamati ya usajili alisema kuwa
uongozi wao chini ya mwenyekiti wa klabu hiyo,
Yusuf Manji hauna nia ya kutaka kumtosa
Ngassa ambapo tayari wameshampatia ofa hiyo
kuhakikisha anasaini mkataba mpya.

Bosi huyo alisema katika ofa hiyo, Ngassa
amepewa masharti mawili muhimu ambapo
ametakiwa kutumia sehemu ya fedha hizo
kumaliza deni lake la benki analodaiwa huku
mshahara wake wa Sh. Mil. 4 ukibaki kama
ulivyo.

Hata hivyo sharti hilo la mshahara linaenda
tofauti na ofa ambayo Ngassa alitaka kupatiwa
na klabu hiyo akitakia alipwe dola 3,500 (Sh. Mil
6.5) kwa mwezi ombi ambalo uongozi wa Yanga
umeligomea.

"Hatuna nia ya kumuondoa Ngassa kuna vitu
ambavyo anakosea, anaongea sana, haangalii
kwamba juhudi zetu tunazozifanya
tumeshampatia ofa hiyo afikirie sasa kama kweli
anataka kubaki hapa," alisema bosi huyo.

"Tumempa hiyo ofa lakini tatizo lake ni moja
anataka mshahara mkubwa sana, kiasi ambacho
ametaka tumpatie ni kikubwa sana kama atakuwa
muelewa katika hili atakubali kusaini."

Ngassa amekuwa akionekana kujuta kwa
maamuzi yake ya kukataa ofa ye kwenda El
Merreikh ya Sudan iliyomtaka wakati akiwa
Simba kwa mkopo akitokea Azam ili tu akipige
Yanga na kukumbana na adhabu ya kuwalipa
Wekundu wa Msimbazi fedha alizosaini awali
kabla ya kukimbilia Jangwani.



Comments