GARETH BALE AENDELEA KUONJA JOTO YA JIWE YA MASHABIKI WA REAL MADRID …washambulia gari lake, wapiga kura aenguliwe kikosini




GARETH BALE AENDELEA KUONJA JOTO YA JIWE YA MASHABIKI WA REAL MADRID …washambulia gari lake, wapiga kura aenguliwe kikosini

Gareth Bale has joined up with the Wales national                team ahead of their upcoming match against Israel

Wakati Gareth Bale alipofunga kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na Spanish Cup msimu uliopita, akawa ameifanyia Real Madird kitu ambacho ni Raul na Ferenc Puskas pekee walioweza kufanya hapo kabla.

Na hata siku moja hakuwahi kuthubutu mshabiki yeyote wa klabu hiyo kulishambulia gari aina Mercedes 180 la Ferenc Puskas mwaka 1959 pindi alipokuwa akitoka mazoezini.

Heshima kama hiyo ilitarajiwa pia kutolewa kwa Gareth Bale lakini kinyume chake, gari lake jeupe aina ya Bentley lilishambuliwa na mashabiki wa Real Madrid wakati mchezaji huyo ghali zaidi duniani akitoka kwenye uwanja wa mazoezini wa klabu hiyo – Valdebebas Training Complex.

Hali hiyo ilitokea mapema Jumatatu mara baada ya kupokea kipigo cha 2-1 kutoka kwa Barcelona katika El Clasico.

Hii si mara ya kwanza wala ya pili kwa Gareth Bale kukutana na adha za namna hiyo kutokwa kwa mashabiki wa Real Madrid na huu ukiwa ni msimu wake wa pili, wingu zito linatanda juu ya hatma ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Wales.

Jumanne iliyopita, asilimia 70 ya mashabiki 8,000 wa klabu hiyo walipiga kura mtandaoni wakitaka Bale aenguliwe kwenye kikosi cha kwanza.



Comments