FM Academia "Wazee wa Ngwasuma" wanarejea tena Mango Garden Ijumaa hii wakitarajiwa kuangusha burudani ya aina yake ikiwa ni wiki mbili tangu wafanye hivyo ndani ya ukumbi huo huo.
Bendi hiyo itakuwa inatumia mwanya wa kutokuwepo kwa Malaika Band ambao ndio wenyeji wa Mango Garden kwa kila siku za Ijumaa.
Msemaji wa FM Academia, Kelvin Mkinga ameiambia Saluti5 kuwa Ijumaa hii bendi yao itakuwa Mango Garden Kinondoni na Jumamosi watakuwa Meeda Club Sinza.
Malaika Band ambao wako kwenye ziara ndefu ya mikoani, watarejea Mango Garden Ijumaa ya tarehe 20 mwezi huu lakini Ijumaa ya tarehe 27 wataukumbia tena ukumbi huo na kwenda kufanya onyesho maalum TCC Club Chang'ombe
Comments
Post a Comment