Fifa yamaliza malumbano ya kombe ka dunia Qatar 2022


BLATANa Augustino Mabalwe,Dar es salaam

Baada ya kuwepo na malumbano kwa muda wa miaka minne kuhusu mashindano ya kombe la dunia mwaka 2022 yatakalofanyika nchini Qatar yafanyikie kipindi gani, sasa shirikisho la soka duniani FIFA limethibitisha kuwa mashindano hayo yataanza kutimua vumbi mwezi Novemba na kumalizika mwezi Desemba mwaka huo.

Mashindano hayo ambayo huwa yanafanyika majira ya kiangazi yamesogezwa mbele ili kuepuka joto ambalo huzidi mpaka nyuzijoto 50 nchini Qatar kipindi hicho cha kiangazi.

Taarifa hii imetolewa hapo jana baada wajumbe wa kamati ya FIFA kukutana huko mjini zurich nchini Switzerland.

Pia michuano hiyo itafanyika ndani ya siku 28 na siyo siku 32 kama ilivyozoeleka awali huku mchezo wa fainali umepangwa kuchezwa siku ya jumapili tarehe 8/12 licha ya kuwa siku hiyo huwa ni sikukuu ya taifa nchini Qatar.

Awali raisi wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) Michelle Plattini alipendekeza fainali ichezwe tarehe 23/12 lakini raisi wa FIFA Sepp Blatter alikataa na kusema itachezwa tarehe 18/12 ili mashindano yachezwe kwa muda mfupi.

Chama cha vilabu barani ulaya (ECA) kinachowakilisha timu 200 awali kilitaka vilabu vilipwe fidia na FIFA kwa kuharibu ratiba za ligi zao lakini shirikisho hilo limekuja juu na kusema hakuna fidia yoyote itakayotolewa na mashindano yataanza tarehe 21 Novemba na na kumalizika tarehe 18 Desemba 2022.

Pia kikao hicho cha jana kiliichagua nchi ya Ufaransa kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2019 kwa upande wa wanawake na kuibwaga korea kusini waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.



Comments