FALCAO AANIKA KUWA ANAWEZA AKATIMKA MANCHESTER UNITED …asema kila mwanasoka anataka uhakika wa namba
Mshambuliaji Radamel Falcao anayekipiga kwa mkopo Manchester United, ameweka wazi kuwa anaweza akatimka Old Trafford kwaajili ya kusaka timu itakayompa nafasi ya kucheza.
Lakini pamoja na kusema hayo, nyota huyo wa Colombia amesema bado ataendelea kuwajibika kwa klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba wake.
Falcao ambaye alikosa michuano ya Kombe la Dunia mwaka uliopita kutokana na kuwa majeruhi, alijiunga na United kwa mkopo akitokea Monaco lakini amekuwa hana uhakika wa namba kwenye kikosi cha Van Gaal.
"Nadhani mwanakabumbu yeyote yule anataka kucheza na anafurahia kucheza," Falcao aliiambia Radio Caracol ya Colombia.
"Ninawajibika kwa asilimia 100 kwa klabu, bado kuna mechi nane mbeleni na lolote linaweza kutokea.
"Hivyo mara tu ligi itakapoisha, tutakaa chini na kufanya tathmini na kufikia lile lililo bora kwangu," alisema Falcao.
Comments
Post a Comment