Licha ya kuibuka washindi hapo jana katika mtanange uliowakutanisha vigogo wawili, mmoja akitokea Ufaransa na mwingine akitokea Uingereza, Chelsea vs PSG, David Luiz ameona sio tabu kuwaomba msamaha mashabiki wa Chelsea kwa kile alichokifanya.
Suluhu ya goli 2-2 ndiyo iliiondoa Chelsea usiku wa jana pale Darajani huku David Luiz akiwa mmoja kati ya wafungaji wa magoli hayo.
Hii ilikuja mara baada ya David Luiz kufunga bao la kusawazisha na kuisaidia PSG kuiondoa Chelsea.
Awali alitangaza kuwa asingeweza kushangilia pindi atajapokuwa darajani kupambana na hiyo timu yake ya awali katika raundi ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya lakini alishindwa kujizuia baada ya kufunga goli zuri.
Kitita cha paund 50 ndicho kilimtoa David Luiz Darajani na kutimkia Ufaransa
David Luiz aliwaomba msamaha mashabiki wa Chelsea kupitia ukurasa wake wa twitter kwamba alikuwa anapambana kwaajili ya kazi yake na hakulenga kuwaumiza
Comments
Post a Comment