Dakika 45 zakatika Taifa, sio Simba wala Mtibwa


Dakika 45 zakatika Taifa, sio Simba wala Mtibwa

???????????????????????????????Na Richard Bakana, Dar Es Salaam
Dakika 45 za kwanza za mcheza wa ligi kuu ya Tanzania bara kati ya Wenyeji Simba SC pamoja na Mtibwa Sugar zimemalizika katika uwanja wa Taifa, Jijijini Dar es Salaam, huku Miamba hao wawili wakishindwa kutambiana kila mmoja.

Katika Dakika 45 zote za mwanzo Mshambuliaji wa Mtibwa ambaye pia amewahi kuichezea Simba, Mussa Hassan Mgosi amekuwa kichomi kwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la wapinzani wao, kitu ambacho kinafanya kipa namba moja wa Wekundu wa Msimbazi, Ivo Mapunda, apate kazi ya kuwa makini kuokoa michomo inayotumwa na mshambuliaji huyo.

Simba nao wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kushitukiza kunako lango la Mtibwa bila mafanikio kwani inaonyesha kuwa safu ya ulinzi ya timu zote imejipanga kuondoa makosa madogomadogo yanayoweza kuigharimu timu yao.

Kabla ya kukutana leo, Timu hizi mbili zilikutana katika mzunguko wa kwanza wa ligi huko Mkoani Morogoro, ambapo zilitoka kwa sare ya 1-1 , Simba wakianza kufunga kupitia kwa Joseph Owino badae Mtibwa wakasawazisha kupitia kwa Henry Joseph, Lakini katika michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyofanyika mwezi Januari, Visiwani Zanzibar, katika hatua ya makundi Mtibwa ilishinda kwa bao 1-0 huku fainali Simba waliichapa Mtibwa kwa mikwaju ya Penati 4-3.

Endelea kufatilia mtandao huu ili kujua nini hatma ya mchezo huu baada ya daada ya dakika 90 kumalizika.



Comments