Malaika Band chini ya Christian Bella leo usiku watatambulisha ngoma yao mpya "Nashindwa" ndani ya ukumbi wa TCC Club Chang'ombe.
Wimbo huo ambao unategemewa kuachiwa rasmi radioni April mosi, tayari umekuwa gumzo katika kila kumbi ambazo Malaika Band wameshatumbuiza.
Mratibu wa onyesho hilo Juma Mbizo, ameiambia Saluti5 kuwa mbali na Malaika kugonga wimbo huo mpya utunzi wake Christian Bella, pia watapiga nyimbo zao nyingine nyingi ikiwemo "Nakuhitaji".
Aidha, Mbizo alisema hata nyimbo maarafu za Christian Bella kama vile "Msaliti", "Usilie" na "Nani Kama Mama" nazo zitaporomoshwa katika onyesho hilo.
Comments
Post a Comment