Mwimbaji nyota wa Jahazi Modern Taarab, Khadija Yussuf "Chiriku" Alhamisi usiku alikwea jukwaa la Mashauzi Classic pale Mango Garden na kusisimua mashabiki kupita maelezo.
Khadija Yussuf akapigiwa wimbo wake "Hasidi Hana Sababu" na kufanya mashabiki wamwagike kwenye 'dancing foor' na kujirusha kwa raha zao.
Kupanda jukwaa la Mashauzi kwa Khadija, kunazidi kuthibitisha kuwa makundi hayo mawili yenye mashabiki wengi, hayana bifu na yanafanya kazi kama ndugu na kwa ushirikiano wa hali ya juu.
Wasanii wengine wa Jahazi waliopanda jukwaa la Mashauzi ni Musa Mipngo aliyekung'uta gitaa la bass pamoja na mpiga solo Emeraa.
Isha Mashauzi ndiye aliyemkaribisha jukwaani Khadija Yussuf na katika kunogesha zaidi tukio hilo Isha pia alimtaka Khadija aimbe kipande kidogo cha "Mapenzi Hayana Dhamana".
Kwa pamoja waimbaji hao wakasema hiyo ni amsha amsha ya onyesho la Baba na Mwana – Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic litakalofanyika Jumapili hii katika ukumbi wa Travertine Hotel.
Comments
Post a Comment