Chicharito asema Real Madrid ni majanga tupu



Chicharito asema Real Madrid ni majanga tupu

IMG_20150329_153906Na Augustino Mabalwe,Dar es salaam

Mshambuliaji Javier Hernadez " "Chicharito" amesema kuendelea kukaa benchi katika klabu ya Real Madrid kunamfanya akose furaha na kukosa kujiamini.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico alijiunga na mabingwa hao wa Ulaya mwanzoni mwa msimu huu akitokea katika klabu ya Manchester United kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mzima.

Katika mkataba huo Real Madrid wanakipengele cha kumsajili moja kwa moja mshambuliaji huyo lakini hana uhakika kama ataendelea kubaki klabuni hapo. "Ninajitahidi kwa asilimia 100 kwenye mazoezi lakini kwenye mechi sichezi,hilo linaondoa kujiamini na ninakosa furaha" alisema Chicharito

Tangu ajiunge na Real Madrid Chicharito amecheza mechi 13 za La Liga na kufanikiwa kufunga magoli matatu na kutoa pasi ya mwisho moja.

Chicharito,26, alijiunga na Real Madrid mara baada ya kukosa namba katika kikosi cha Louis Van Gaal na pia kuwasili kwa mshabuliaji Radamel Falcao kulichangia kwa kiasi kikubwa.

Mchezaji huyo ambaye mkataba wake katika klabu ya Manchester United unaisha June 2016 alifunga katika mechi ya kirafiki ya juzi jumamosi ambayo ilimalizika kwa Mexico kushinda 1-0 dhidi ya Ecuardo.



Comments