BASATA yamkabidhi Bendera Mshindi wa Airtel Trace Music,


BASATA yamkabidhi Bendera Mshindi wa Airtel Trace Music,

????????Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA), Nsao Shalua (kushoto), akikabidhi bendera ya taifa kwa
mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi kwa ajili ya
kwenda kuiwakilisha nchi katika fainali za Afrika za Airtel Trace
Music Stars zitakazofanyika Jumamosi Machi 28, nchini Kenya na
kushirikisha nchi 13, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye
ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati),
ni Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga.

Barasa la Sanaa Tanzania leo limemkabithi bendera mshindi wa shindanola Airtel Trace Music Stars Bwana Nalimi Mayunga anayeondoka leo nchi

kwenda kuhudhuria mashindano ya Airtel Trace Afrika yatakayoshirikisha
washiriki toka nchi 13 barani Afrika yanayofanyika nchini Kenya siku
ya Jumamosi tarehe 28 March 2015.

Mayunga aliibuka mshindi katika kinyanganyiro cha kusaka Wakali wa
vipaji vya mziki kupitia shindano la Airtel Trace Music
lililozinduliwa na kampuni ya Airtel Tanzania Mwaka Jana mwezi wa kumi
na kushirikiksha washiriki mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali nchini
ambapo fainali ya kumsaka mshindi ilifanyika mwanzoni mwa mwezi wa
februari na kumwezesha Mayunga kuwashinda washindani wengine watano na
katika fainali hizo na kuondoka na kitita zawadi ya shilingi million
50.
Akiongea wakati wa kukabithi bendera hiyo, Mkurugenzi wa ukuzaji sanaa
na Masoko wa BASATA bi Nsao Shalua alisema"  kwanza tunachukua fulsa
kuwapongeza Airtel kwa kuanzisha shindano hili na kwa kufata taratibu
zote za kuratibu mashindano.  Airtel leo wameonyesha mfano kwa kumleta
mshindi hapa ofisini, kuaga rasmi na kupatiwa kibali cha kusafiri
kutoka baraza la sanaa Tanzania kitu ambacho hakifanywi na makampuni
mengi na hata wasaani wengi nchini. Huu ni mfano wa kuigwa na natoa
wito kwa watu wote wanaoondoka nchini kwaajili ya kwenda kufanya
shughuli za sanaa kuhakikisha wanafata utaratibu kwa kutufahamisha na
kupata hati maalumu ya kushiriki shughuli na kuiwakilisha nchi yetu
nje ya nchi.
SONY DSCMshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi akiwa ameshika
bendera mara baada ya kukabithiwa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na
Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa.

(BASATA), kwaajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya muziki ya
Airtel Trace Music Stars yatakayofanyika Jumamosi hii nchini Kenya
Aidha napenda kumpongeza Mayunga kwa kuibuka kuwa mshindi na kupata
nafasi ya kuwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Afrika, tunapenda
kumwomba atumie fulsa hii vizuri na kwa kufanya hivyo basi tunaamini
atafanya vyema. Tunamtakia safari njema na mashindano mema, tunaamini
Mayunga atatuwakilisha vyema na kutangaza nchini yetu katika angaza za
muziki kwa ujumla

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga alisema" Leo
tunamuwezesha Mayunga kwenda kushiriki na kuiwakiisha nchi yetu katika
mashindano ya Afrika Tunamwezesha kujiwekea umaarufu na kuonyesha
kipaji chake kwa wadau wa ndani na nje ya nchi, pamoja na Mayunga
tunawawezesha vijana wengi barani Afrika kwa ujumla kuzifikia ndoto
zao. Mashindano haya yatafanyika siku ya Jumamosi , jijini Naivasha
Kenya ambapo washiriki kutoka nchi 13 barani Afrika watachuana vikali.
Mshindi wa Airtel Trace Afrika atapata nafasi ya kwenda nchini
marekani na kupata mafunzo kutoka kwa mwanamuziki wa miondoko ya R&B ,
Akon na kuweza kurekodi nyimbo zake.

Natoa wito kwa watanzania kumpigia kura Mayunga kwa ku  tuma SMS,
yaani ujumbe mfupi andika neno YUN kwenda 15594,  Alhamisi ni siku ya
mwisho ya kupiga kura, asiliimia 25 ya ushindi inatoka kwenye kura
yako hivyo kura yako ni ya muhimu sana. Aliongeza Aneth.

Akiongea mara baada ya kukabithiwa bendera Malimi Mayunga alisema"
namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufikia hatua hii,
nawaahidi watanzania kuwawakilisha vyema, pamoja na hayo nawaomba sana
watanzania waniunge mkono kwa kunipigia kura ili nipate nafasi ya
kuweza kuibuka kuwa mshindi. Hii kwangu ni nafasi ya pekee sana na
namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha na

Airtel kwa kuwawezesha vijana kama mimi kuonyesha vipaji vyao na
kuzifikia ndoto zao kupitia mashindano mengi kama haya

Mashindano ya Airtel Trace Music Star yalianzishwa kwa lengo la
kuonyesha vipaji vya vijana kimuziki na nakuwapatia fulsa ya kukua
kimuziki.



Comments