Mario Ballotel siku ya jummane aliweza kutoa kali ya wiki mara baadaya kuwaponda wale wote wanaomfuatilia na kumsema kuwa hana lolote uwanjani kwasasa, na hili alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram kupitia video aliyojirekodi mwenyewe akiwataka wakae kimya.
Akiongea kiukaribu zaidi na camera yake Ballotel alisema
"Unanijua? Ushawahi kukutana nami uso kwa uso? Unajua ni vitu gani nimevipitia katika maisha yangu? Umenijua tu kwa kuniona uwanjani nikicheza mpira, kwahiyo Kaa Kimya!!! " Ballotel alitamka maneno hayo akiwa katika muonekano wenye hasira kali.
Muitaly huyo (24) alitamka maneno hayo kutokana na malalamiko ya wengi juu ya uwezo wake uwanjani kuonekana kama umeporomoka, kumbuka Mario alisajiliwa na Liverpool akitokea Ac Milan kwa kitita cha £16million.
Hadi sasa Ballotel ameifungia timu hiyo magoli manne tu katika mechi 20 alizocheza ndani ya timu hiyo.
Comments
Post a Comment