Baada ya Chelsea kutupwa nje kwenye Ligi ya Mabingwa huku mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic akisema wapinzani hao walikuwa kama kundi la watoto wanaodeka uwanjani, picha za mzaha zimetawala mitandaoni kuwadhihaki vinara wa Premier League.
Picha kadhaa zimetupiwa mitandaoni zikiwa zimekarabatiwa na kuweka nyuso za watoto wachanga kwenye vichwa vya wachezaji wa Chelsea pamoja na kocha wao Jose Mourinho. Picha zingine zilionyesha wachezaji hao wakiwa wamefungwa nepi.
Comments
Post a Comment