Arsene Wenger: Monaco hawakustahili kushinda kabisa


Arsene Wenger: Monaco hawakustahili kushinda kabisa
Arsene+WengerNa Amplifaya Amplifaya
Kocha mkuu wa wa timu ya Arsenal Arsene Wenger amesema Monaco hawakustahili kabisa kuingia hatua ya robo fainali baada ya kushindwa kufikisha idadi ya mabao husika (aggregate) katika mchezo huo Arsenal walikuwa wageni katika uwanja wa Monaco.
Monaco ilijiweka katika mazingira mazuri zaidi katika uwanja wa Emirates mara baada ya kushinda goli 3-1 na wao kufungwa goli 2-0 hapo jana nyumbani kwao.
Akizungumza na waandishi wa habari Arsene Wenger aliulizwa kama Monaco walistahili kushinda naye alisema "hapana na sidhani kama walistahili, tulipata nafasi nyingi sana za kufunga japo tulikosa tofauti na wao ambao walikuwa nazo chache.
Wenger alikuwa na mtazamo tofauti kabisa na Per Mertesacker, mchezaji aliyeibuka bingwa wa kombe la dunia na timu yake ya Ujerumani mwaka jana kwa kusema kuwa Monaco ndiyo walistahili kushinda mechi hiyo kutokana na uwezo mzuri waliouonesha hapo jana.
Pia alizidi kusema kuwa "tulikuja hapa na tulitumia kila mbinu lakini tulishindwa kufunga licha ya nafasi mbili ambazo tulizipata natukazitumia kufunga, tunajutia sana hasa mchezo wetu wa kwanza"
Arsenal iliwabidi kujipatia ushindi wa goli 3-0 dhidi ua wenyeji ili kuendelea na raundi ijayo ambayo ni ya mtoano wa hatua ya robo fainali lakini Monaco walihakikisha hawaruhusu magoli hayo yote yanapatikana kutoka kwao usiku huo wa jana.
Ligi hiyo ya mabingwa barani ulaya itaendelea tena hii leo ambapo miamba wa soka nchini Hispania Fc. Farcelona watawakiribisha Manchester City katika uwanja wa Camp Nou halikadhalika Borussia Dortmund watakutana na Juventus kutoka Italy majira ya saa 4:45 usiku wa leo.


Comments