Arsenal wamepoteza kwa ncha nafasi ya kufanya maajabu kwenye Champions League baada ya kushuhudia bao zao 2-0 dhidi ya Monaco kwenye uwanja wa Stade Louis II zikishindwa kuwavusha kwenda hatua ya robo fainali.
Wikiwa wamefungwa 3-1 Emirates Stadium katika mchezo wa kwanza, Arsenal walihitaji ushindi wa bao 3-0 ili kusonga mbele na matumaini ya wageni yaliongezeka baada ya Ramsey kufunga bao la pili dakika ya 79.
Bao la kwanza la Arsenal liliwekwa kimiani na Giruod katika dakika ya 36 na kama vijana wa Arsene Wenger wangefanikiwa kupenya, basi ingekuwa timu ya kwanza kufanya hivyo tangu mwaka 1969 wakati Ajax ilipotoka nyuma kwa tofauti ya bao mbili kwenye uwanja wao wa nyumbani na kusonga mbele baada ya mchezo wa marudiano ugenini kwenye European Cup.
Comments
Post a Comment