Aliyeiua Simba SC Dar fiti kuivaa Mgambo J’pili


Aliyeiua Simba SC Dar fiti kuivaa Mgambo J'pili

Rafael Daud wa CityNa Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kiungo fundi katika kikosi cha Mbeya City, Rafael Daud atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Mgambo JKT  Uwanja wa Sokiner, Mbeya Jumapili, imefahamika.
Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa Mbeya Cioty FC, kiungo huyo aliyekuwa chachu ya ushindi wa 2-1 wa timu hiyo ya Jiji la Mbeya dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa mwezi uliopita, amepona majeraha aliyopata kwenye mechi iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar FC iliyochezwa Manungu, Turiani mkoani Morogoro Jumapili.

Daktari mkuu wa City, Joshua Kaseko amekaririwa na katika mtandao wa City leo akieleza kuwa  Rafael alipata majeraha kwenye kifundo cha mguu 'enka' katika mchezo huo ulkiomalizika kwa sare ya 1-1, jambo lililosababisha nyota huyo kulazimika kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Mapunda kufuatia  maumivu kwenye kifundo cha mguu.

"Atakuwa fiti kuivaa Mgambo Jumapili, ni matarajio yetu hasa baada ya maendeleo mazuri  kufuatia matibabu ya siku hizi tatu, ni mmoja kati ya wachezaji hodari ambao wana nguvu kubwa kwenye kikosi chetu uwapo wake  Jumapili hii utaongeza nguvu katika kuusaka ushindi ambao ni muhimu kwetu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri  katika msimamo wa ligi," umeeleza mtandao wa City.

Mbeya City FC, inayonolewa na kocha bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Juma Mwambusi, iko nafasi ya pili kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo.



Comments