Zawadi Kilimanjaro Marathoni 2015 zatangazwa, Watatu wapelekwa Kenya kujifua zaidi



Zawadi Kilimanjaro Marathoni 2015 zatangazwa, Watatu wapelekwa Kenya kujifua zaidi

kili-marathon-2013-4-620x400Waratibu wa michuano ya mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathoni 2015, wametangaza gharama na zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mchezo huo ambao kilele chake itakuwa Machi 1 Mjini Moshi.

Akizungumza na Shaffihdauda.com Mkurugenzi wa Executive Solution ambao ndio waratibu wa mashindano hayo, Agley Marealle ametaja zawadi kwa washindi wa mbio za kilomita 42, Kilomita 21 , Kilomita 5 na zile za walemavu.

"Kwenye mbio za kilomita 42 zawadi jumla ni Tsh. Milioni 20, ambapo mshindi wa kwanza atachukua Milioni nne, wa pili milioni mbili, wa tatu milioni moja, wan ne laki sita, na kuendelea hadi mshindi wa 10, Kwenye nusu Marathoni mshindi wa kwanza atapata Milioni mbili, wa pili milioni moja, Wa tatu laki tano, wan ne laki nne na nusu, W tano laki tatu na kuendelea hadi mshindi wa 10, Kwenye mbio za walemavu za kilomita 10, Mshinndi wa kwa atabeba laki tano, Wa pili laki nne, wa tatu laki tatu, Wan ne laki mbili, Wa taNO atachukua laki moja na nusu, pia walemavu watapata viti vya kutembelea" Amesema Mkurugeni huyo.

Mbio hizo inatazamiwa kuwa ni kubwa zaidi Duniani za kitarii, huku kwa Tanzania ikiwa ni Tukio kubwa zaidi la kimichezo.

Hata hivyo baada ya Tanzania kuendelea kufanya vibaya katika mbio za kimataifa za
Kilimanjaro Marathoni klabu ya Riadha ya Holili (HYAC) ya mkoani
Kilimanjaro imelazimika kuwapeleka wanariadha wake watatu nchini Kenya
kwa ajili ya mazoezi ya mbio ndefu za Kilometa 42 .kilimanjaro-marathon-24



Comments