Yusuf Manji sasa hii sifa


Yusuf Manji sasa hii sifa
DSCN3000
HATIMAYE timu ya Yanga imekuwa ya kwanza Tanzania inayolipa posho za wachezaji vizuri kuliko timu zingine zote za ligi kuu Tanzania bara. 
Awali Yanga ilikuwa ikiwapa posho wachezaji wake sh 70,000 kwa mechi wanazoshinda kwa wale wanaoingia Uwanjani na 35,000 kwa wale ambao hawakupangwa.

Kupitia kwa mwenyekiti wake, Yusuf Manji timu hiyo imefanya kufuru na sasa kila mechi  watakayoshinda wachezaji 18 watapata posho ya Sh 140,000 na kwa wale ambao hawakuvaa  jezi watapata sh 98,000 
Kwa maana hiyo Yanga itakuwa inawalipa wachezaji wake vizuri kuliko simba na Azam FC…
Awali timu ya Azam FC ndio ilikuwa inalipa vizuri ikiwa inalipa sh. 130,000 kwa mechi wanazoshinda. Huku Simba wakilipa sh, 50,000 tu kwa game wanazoshinda.


Comments