Na Amplifaya Amplifaya
Beki mahiri anayeweza kucheza nafasi ya kiungo Mbuyu Twite kesho atakosa moja kati ya mechi ngumu zaidi kati ya Yanga na Mbeya City itakayochezwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ni katika mwendelezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Twite atakosa mechi hiyo hapo kesho kutokana na kupata kadi ya njano katika mchezo uliopita dhidi ya Prison Fc na kufanya afikishe idadi ya kadi 3 za njano, kumbuka Yanga walishindwa goli 3-0 dhidi ya wenyeji.
Kuna uwezekano mkubwa wa Juma Abdul kucheza nafasi yake utakuwepo kama mbadala pia katika nafasi ya Ulinzi wa kiungo Salum Telela atasimama kuongoza timu.
Moja kati ya vitu ambavyo Yanga watavikosa kutoka kwake ni uhodari na kipaji chake cha kurusha mipira ambayo mara nyingi imekuwa ikiisaidia timu kuwa na nafasi nzuri ya kutengeneza mabao, na mipira hiyo huonekana kama imepigwa na mguu.
Hans Van Der Pluijm amesema kwamba kukosekana kwa Twite hakuna tija sana sababu mbadala wake upo.
"Ni sawa amekosekana lakini hakuna tabu sana sababu tuna vijana wengine ambao watacheza nafasi yake kama mbadala" Hans alisema hayo
Comments
Post a Comment