YANGA wameendelea kujikita kileleni mwa ligi kuu soka Tanzania bara kufuatia kuichapa Mbeya City fc mabao 3-1 katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa jioni ya leo uwanja wa CCM Sokoine, Mbeya.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Simon Msuva katika dakika ya 18 alipounganishwa kwa kichwa krosi ya Niyonzima.
Mrisho Ngassa alifunga goli la pili dakika ya 59 baada ya kipa wa City David Buruhani kuuwahi mpira wa Oscar Joshua, lakini akamsubiri Ngassa ili ampige chenga, 'Anko' hakufanya makosa akatia mpira kambani.
Dakika ya 78 kona iliyochongwa na Haruna Niyonzima iliunganishwa kwa kichwa na Amissi Tambwe aliyefunga goli la tatu.
Bao la Mbeya City lilifungwa dakika ya 68 na Peter Mapunda akiunganisha krosi kutoka wingi ya kulia iliyochongwa na Deus Kaseke.
Kwa matokeo hayo, Yanga wamefikisha pointi 31 baada ya ya kushuka dimbani mara 14.
Wameshinda mechi 9, wametoa sare mechi 4, wamefungwa mechi 2. Wamefunga magoli 21 na kufungwa 8, tofauti ya mabo ya kufunga na kufungwa ni 13.
Muda Azam fc wapo uwanjani kuchuana na Prisons uwanja wa Chamazi.
Kama Azam fc watashinda mechi hii watafikisha pointi 29, pointi mbili nyuma ya Yanga na kama watapoteza bado wataendelea kushika nafasi ya pili.
Comments
Post a Comment