Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi Botswana leo
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho, Dar Young Africans wameendelea na mazoezi ya mwisho mwisho nchini Botswana kujiandaa na marudiano dhidi ya wenyeji BDF XI itayopigwa kesho kutwa, februari 28 mwaka huu.
Yanga chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm wapo katika morali ya ushindi na wachezaji wote waliosafiri wapo salama.
Bahati nzuri kwa Yanga ni kwamba wataingia uwanjani wakiwa na faida ya mabao 2-0 waliyovuna uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, februari 14 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mabao yote siku hiyo yalifungwa na Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe.
Ili kusonga mbele Yanga wanahitaji ushindi, suluhu au sare ya aina yoyote ile au wasifungwe zaidi ya goli 1-0.
Kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm (kushoto) baada ya mazoezi akiwa ameketi na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' kwenye basi walilotumia kutoka Hotelini kwenda uwanjani.
Habari njema kwa wapenzi wa soka nchini ni kwamba mtanange huo utaoneshwa moja kwa moja 'Live' kipitia kituo cha Televisheni cha Azam TV kuanzia majira ya saa 2:30 usiku.
Mechi ya kwanza Dar es salaam, Yanga walipiga marufuku chombo chochote cha TV kuonesha mechi hiyo, lakini safari matangazo yatapokelewa na Azam TV moja kwa moja kutoka Botswana na kuwafikia Watanzania wote.
Comments
Post a Comment