Watu wa Mwanza kweli mliwahujumu Kagera Sugar?



Watu wa Mwanza kweli mliwahujumu Kagera Sugar?
KAGERA-VS-SIMBA-390x305
"Tumeshinda bao 1-0, lakini sijaridhishwa sana na kiwango cha wachezaji wangu, wanapigiana pasi nyingi kwenye eneo lao, wanapofika eneo la mpinzani wanashindwa kupiga hesabu vizuri za kupenya ngome ya ulinzi".
"Umeona jinsi tulivyowazidi Polisi Moro kiuchezaji, lakini naamini ni washindani wa kweli, naenda kukaa chini na wachezaji wangu ili tuendelee kufanya vizuri" Amesema Jackson Mayanja.
Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Morogoro katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyopigwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Awali Kagera Sugar walichangua kutumia uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kufuatia dimba lao ka Kaitaba kuwa katika marekebisho.
Walifungwa mechi tatu mfululizo, 1-0 na Mbeya City, 3-0 na Azam fc na 2-1 dhidi ya Ndanda fc.
Baada ya hapo uongozi wa klabu hiyo ukaamua kuhama uwanja huo na kwenda Kambarage Shinyanga kwa madai kuwa wanahujumiwa na wenyeji wa mwanza.
Baada ya vipigo hivyo walisafiri kwenda Mbeya walikotoa sare ya 1-1 na Prisons na wakarudi Kambarage ambako wameshinda mechi zote tatu walizocheza.
Waliwafunga 1-0 Mgambo JKT, wakainyuka 1-0 JKT Ruvu na jana wameshinda 1-0 dhidi Polisi Morogoro.
Ukiangalia matokeo haya, unaweza kuamini kuwa hujuma zipo katika mchezo wa soka nchini.
Kwasasa Kagera wapo nafasi ya tatu kwa pointi 24, pointi 4 nyuma ya Vinara Yanga, na pointi 2 nyuma ya Azam fc wanaoshika nafasi ya pili.


Comments