Watakatifu wamfanyia kitu mbaya Adam Lallana


Watakatifu wamfanyia kitu mbaya Adam Lallana
25F46B5C00000578-0-image-a-5_1424635251816
Adam Lallana (kushoto) alizomewa na mashabiki
MENEJA wa Liverpool, Brendan Rodgers amekiri kushangazwa na jinsi nahodha wa zamani wa Southampton, Adam Lallana alivyopokelewa vibaya akirejea katika dimba la St Mary kwenye mechi ya ligi  ambayo Liverpool walishinda 2-0 jana.
Kiungo huyo aliyekaa Southampton kwa miaka 14, alijiunga na Liverpool majira ya kiangazi mwaka jana na jana alizomewa na mashabiki wa nyumbani kama ilivyokuwa pia kwa Dejan Lovren aliyeondoka klabuni hapo kujiunga Anfield mwishoni mwa msimu uliopita.
Mshambuliaji Rickie Lambert ambaye alikuwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba, ingawa hakucheza, yeye alipokelewa vizuri.


Comments