Kundi la Wakali Wao Modern Taradance chini yake Thabit Abdul "Mkombozi" Jumatatu mchana walifichua rasmi vyombo vyao vipya kabisa vyenye thamani ya mamilioni.
Tukio hilo lilifanyika kwenye kambi yao Mchili Pub Kinondoni na kushuhudiwa na wadau kadhaa wa muziki.
Thabit Abdul ambaye ndiye mmiliki wa kundi hilo akaiambia Saluti5 kuwa vyombo hivyo vimegharimu milioni 24.
"Nashukuru sana, mtu mwenye moyo wa kunisaidia amejitoa muhanga na kuniwezesha kupata vyombo vipya kabisa, huu ni ukombozi mkubwa kwa kundi letu," alisema Thabit.
Thabit Abdul amewataka wapenzi wa Wakali Wao kukaa mkao wa kula kwani kuna mambo makubwa zaidi yanakuja. "Huu ni mwanzo tu, mambo mengi makubwa yanakuja."
Tazama baadhi ya picha zilizopigwa na kamera ya Saluti5 Jumatatu mchana, achana na zile zilizosambazwa na bendi hiyo kupitia Facebook. Mzigo kamili ni huu hapa.
Comments
Post a Comment