Wakiwa na vyombo vyao vipya kabisa, Wakali Wao Modern Taradance chini yake Thabit Abdul, wanatarajiwa kufanya onyesho la aina yake kwa wakazi wa Kigamboni ndani ya ukumbi wa CCM Jumamosi hii.
Waandaji wa onyesho hilo, Posh Entertainment wameiambia Saluti5 kuwa mbali na Wakali Wao, pia kutakuwa na wasanii waalikwa ambao ni Mauwa Teggo wa Coast Modern Taarab na Jack Simela mkali wa mchiriku kutoka Jagwa Music.
Moja ya vivutio vinavyotarajiwa kupamba onyesho la Wakali Wao, ni vyombo vyao vipya vya muziki vilivyozinduliwa wiki hii.
Kundi hilo linatamba na albam zake mbili "Kalieni Viti Msikalie Umbeya" na "Mtu Mzima Ovyo" ambazo kwa pamoja zinategemewa kuwasha moto mkubwa wa burudani ndani ya CCM Kigamboni.
Comments
Post a Comment