VAN GAAL ASEMA ROONEY HAJAWAHI KUMLALAMIKIA KUHUSU KUCHEZESHWA KAMA KIUNGO


VAN GAAL ASEMA ROONEY HAJAWAHI KUMLALAMIKIA KUHUSU KUCHEZESHWA KAMA KIUNGO

Rooney went down a moment after and several of the              Preston players were unhappy with his actions

Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema hajawahi kupata malalamiko yoteyote kutoka kwa nahodha wake Wayne Rooney juu ya kupangwa kwake nafasi ya kiungo.

Van Gaal amedai Rooney yuko na furaha kucheza kama kiungo ingawa anaweza akamtumia kama mshambuliaji huko baadae.

"Naamini Rooney ni mshambuliaji bora lakini kwa sasa nitaendelea kumtumia kama kiungo ili kuweka uwiano wa timu," anaeleza kocha huyo asiyekubali kuyumbishwa katika kile anachokisimamia.

"Ana furaha kucheza kama kiungo vingenevyo angeshanifuata na kunieleza. Hakuwahi kufanya hivyo, siku zote amekuwa rafiki kwangu. Anataka kufanya kile ninachotaka na hiyo ndiyo hali halisi.

"Lakini huwezi kujua, yeye ni binadamu na pengine ulimwengu mzima unapoandika kuwa anapaswa kuchezeshwa kama mshambuliaji, anaweza akabadilika kifikra."



Comments