VAN GAAL AMFANYIA KITU MBAYA JUAN MATA KAMA ALIVYOFANYA MOURINHO



VAN GAAL AMFANYIA KITU MBAYA JUAN MATA KAMA ALIVYOFANYA MOURINHO

Juan Mata is increasingly finding himself sidelined                at Manchester United despite his impressive record

Hatma ya kiungo mshambuliaji wa Manchester United Juan Mata ndani ya klabu hiyo iko mashakani na ni wazi kuwa nyota huyo wa Hispania anaweza kutimka kama ataendelea kukosa nafasi ya kudumu kwa kocha Louis van Gaal.

Mata aliwasili Old Trafford miezi 13 iliyopita kwa ada iliyovunja rekodi ya klabu pauni milioni 37.1 ukiwa ni usajili uliofanywa na kocha aliyetimuliwa David Moyes.

Baada ya kuanza kutumikia United kwa kusuasua kutokana na kutokuwa fiti ipasavyo, Mata akacharuka baadae na kufunga magoli sita katika mechi sita za mwishoni wa msimu.

Lakini ujio wa Van Gaal umetibua njozi zake na sasa Mata anakutana na enzi za kiza kama ilivyokuwa katika maisha yake ya Chelsea chini ya Jose Mourinho.

The £37.1million signing from Chelsea had similar              problems at his former club with manager Jose Mourinho

Mata alikuwa ndio mpishi wa magoli ya Chelsea yakiwemo ya Champions League mwaka 2012 ambao mchezaji huyo alitengeneza magoli mawili kwenye hatua ya fainali bila kusahau fainali ya kombe la FA Wembley Stadium pale Mata alipopika bao la kwanza.

Mwaka 2013 Mata akapiga kona iliyozaa bao lililochangia ushindi kwenye fainali ya Europa League. Akafunga magoli 20 na kutegeneza 35 katika mashindano yote ya msimu huo.

Licha ya kuwa mchezaji bora wa Chelsea kwa misimu miwili mfululizo, Mata akaangukia pua mara tu Jose Mourinho aliporejea Stamford Bridge.

Akakosa nafasi kwa Mourinho, Moyes akamtwaa na kumpa matumaini mapya lakini Van Gaal anamrudisha tena kwenye zama za kusugua benchi licha ya wachambuzi wengi wa soka kuamini kuwa Mata ndio injini ya kuipa United nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Mata finds a place on the bench away at West Brom and              he rarely makes it into a fully fit starting XI

Wakati makocha Andre Villas-Boas, Roberto Di Matteo na Rafa Benitez walikuwa mashabiki wa Mata ndani ya Chelsea, Mourinho 'akampuuza'. Na wakati Moyes aliona umuhimu wa kupata huduma ya Mata, Van Gaal anamtumia kama mchezaji wa akiba.



Comments