Na Amplifaya Amplifaya
Jamhuri Kiwhelo almaarufu kama Joseph Mourinho wa Bongo, jina ambalo alipewa na mashabiki wa hapa Tanzania kutokana tu na namna ya uongeaji wake wa maneno mengi, tumeweza kushuhudia akifanikisha kuipandisha Mwadui Fc ligi kuu vodacom.
Julio alifanikisha ndiyo zake baada ya kuifunga timu ya Polisi Tabora katika mchezo ambao walishinda goli 4-3 na kufikisha pointi ambazo zilitoa kibali cha moja kwa moja kwa Mwadui kuingia ligi kuu msimu ujao. Kumbuka Mwadui ilikosakosa kidogo kupanda ligi kuu kutokana na pointi za mezani ambazo walizipata Stand United na kuipandisha ligi kuu huku Mwadui Fc ikibaki.
Mapema February mwaka huu mara baada ya kuipandisha timu Ligi kuu Julio ametuonesha asili ya Utanzania wetu kukosa long time planning hasa kwa makocha na viongozi katika timu zetu za Kitanzania.
Unapokuwa unasonga ugali kwenye sufuria hakuna budi ya kutokuzima moto maana kile kipikwacho hakitaiva kabisa, pia soccer la sasa halihitaji zimamoto kwani itachangia kudhorotesha viwango na overall performance ya timu mzima bali inatakiwa uwashwe moja kwa moja.
Huu ni muda ambao nilitegemea kumuona Julio akiweka planning nzuri kushiriki ligi kuu msimu ujao na kama mwalimu wa Mwadui Fc. Ni muda ambao alitakiwa kukaa na kupanga mikakati hasi huku akishirikiana na viongozi wake wa kuu kwaajili ya kutengeneza njia nzuri za kukomaa ili kuwania kombe la Vodacom kwa msimu ujao.
Kitendo cha yeye kuiacha timu kwasasa na kutimkia Cost Union hakutakiwa afanye vile!
Hebu iangalaie Mwadui ya sasa ambayo nina imani kabisa haina kikosi cha pili au Timu B ijulikanayo kama U(20) na kwa sheria na kanuni za soka kila timu inatakiwa kuwa na U20 ambayo itakuwa kama hazina ya timu A kwa hapo baadae na hili linafanywa na vilabu vyote duniani.
Ni muda ambao ungetumika kuinoa timu ya vijana chini ya miaka 20 na angepata hata fursa ya kuvipiga bao vilabu vikubwa kama Simba au Yanga au Azam ambavyo vipo busy na ligi kuu kwa wakati huu pamoja na michuano mingine ya kimataifa kwa Azam na Yanga.
Kumbuka Mwadui sasa wachezaji wake wapo huru kwenye likizo ya muda mrefu kidogo. Ulikuwa ni wakati mwafaka sasa kwa Julio kuijenga Mwadui Fc, kutafuta wachezaji wapi wangemfaa na kuandaa kikosi cha vijana kwa likizo hii iliyopo.
Comments
Post a Comment