KOCHA wa Southampton, Ronald Koeman anakusudia kumuadhibu Sadio Mane kufuatia mshambuliaji huyo kuchelewa kufika katika mechi waliyopoteza 2-0 dhidi ya Liverpool.
Mane alikuwepo katika kikosi kilichowakabili wakali wa Merseyside kwa kufika baada ya nusu saa kupita kutoka muda waliopanga kufika, saa saba mchana.
Pia mashambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal anakabiliwa na adhabu nyingine ya kutozingatia muda.
Mane akichuana na kiungo wa Liverpool Liverpool, Philippe Coutinho (kulia)
"Alichelewa kwa dakika 25-30 kabla ya mechi", amethibitisha Koeman.
"Tuna kanuni na maelekezo kwa wachezaji. Kila mtu anaweza kuchelewa siku moja asubuhi, lakini huwezi kuchelewa kufika saa saba wakati unacheza dhidi ya Liverpool.
"Hakutoa maelezo? Maelezo hayo ni baina ya kocha na mchezaji, lakini alichelewa.
'Siwezi na sikubaliani na hilo. Kama ni kulipa faini alipe tu"
Comments
Post a Comment