Tottenham imenusurika na kipigo cha nyumbani baada ya kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya West Ham kwenye mchezo mkali wa Premier League.
Hadi dakika ya 81, West Ham walikuwa mbele kwa bao 2-0 kufuatia magoli ya Cheikhou Kouyate dakika ya 22 na Diafra Sakho (dakika ya 62) na ilionekana wazi kuwa Tottenham wanadondosha pointi tatu.
Beki wa pembeni Danny Rose akapunguza bao moja zikiwa zimesalia dakika 9 na kuamsha ari ya Tottenham.
Dakika tisini za kawaida zikaisha West Ham wakiwa mbele lakini dakika ya mwisho ya muda wa majeruhi (90+5) kiungo wa West Ham anayeichezea klabu hiyo kwa mkopo Alex Songo akamdondosha Harry Kane ndani ya 18 na kuwa penalti.
Harry Kane akapiga mkwaju huo wa penalti lakini kipa Adrian akapangua kabla mpira haujarejea tena kwa Kane na kufunga kirahisi bao la kusawazisha.
Tottenham (4-2-3-1): Lloris 7; Walker 5.5, Dier 5, Vertonghen 5.5, Rose 6.5; Mason 5 (Chadli 80, 6), Bentaleb 5.5, Townsend 5 (Soldado 60, 5.5), Dembele 4.5 (Eirksen 46, 6), Lamela 5.5; Kane 7.
West Ham (4-3-3): Adrian 5; Jenkinson 6, Tomkins 6, Reid 6, Cresswell 6.5; Song 6, Noble 7 (Cole 68, 5 [Collins 87, 5.5]), Kouyate 7; Valencia 6 (Jarvis 74, 5.5), Sakho 6.5, Downing 6, Sakho 6.5.
Comments
Post a Comment