TFF yaomboleza kifo cha Christopher Alex



TFF yaomboleza kifo cha Christopher Alex

Christopher AlexRais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF amepeleka salamu za rambirambi kwa familia ya Alex Bw.Massawe, kufuatia kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Star) na klabu ya Simba SC, Christopher Alex kilichotokea jana mjini Dodoma.

Christopher Alex Massawe aliwahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) mwanzoni mwa miaka ya 2000's na kwa mafanikiko makubwa huku pia akiwa tegemeo katika klabu yake ya Simba SC.

Katika salam zake kwa familia ya Massawe, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania Rais Malinzi amewapa pole wapenzi wa mpira wa miguu nchini  katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.



Comments