Taifa Stars, Zimbabwe zala sahani moja COSAFA



Taifa Stars, Zimbabwe zala sahani moja COSAFA

ulimwengu

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa starsimepangwa kwenye kundi A katika michuano ya kombe la COSAFA yanayotarajia kufanyika nchini Afrika kusini mwezi mei mwaka huu.

Taifa stars wamepangwa sambamba na Zimbabwe, Lesotho na Namibia katika michuano hiyo ambayo Taifa stars imealikwa kushiriki pamoja na Ghana.

Makundi ya michuano hiyo inayoshirikisha timu za taifa za kusini mwa Afrika yamepangwa usiku wa jana  ambapo yamewekwa katika makundi mawili.

Vinara wa kila kundi wataingia hatua ya robo fainali ambapo watajumuika na timu nyingine sita ambazo ni Malawi, Zambia, Afrika kusini, Botswana, Ghana na Msumbiji.

KUNDI A
A1 – Namibia
A2 – Lesotho
A3 – Zimbabwe
A4 – Tanzania

KUNDI B
B1 – Seychelles
B2 – Madagascar
B3 – Mauritius
B4 – Swaziland



Comments