Swansea imetibua mbio za Manchester United kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa 2-1 katika mchezo uliopigwa Liberty Stadium.
Wenyeji wakatoka nyuma na kufunga mabao mawili kupitia kwa Ki Sung-Yueng na Bafetimbi Gomis na kupata pointi tatu muhimu zilizoiporomosha United hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Swansea kuifunga United mara mbili ndani ya msimu mmoja wa Ligi Kuu baada ya kuifunga kwa idadi kama hiyo kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Old Trafford.
United ilifunga bao lake pekee katika dakika ya 28 kupitia kwa kiungo wake wa Kihispania Ander Herrera, hili likiwa ni bao lake la pili kwenye Ligi Kuu tangu ajiunge na timu hiyo majira ya kiangazi.
Hata hivyo furaha ya United ilidumu kwa dakika mbili tu kabla ya Ki Sung-Yueng hajaisawazishia Swansea kufuatia krosi maridadi ya Jonjo Shelvey.
Kipindi cha pili United iliudhibiti mchezo kwa muda mrefu hadi pale Gomis alipofunga dakika ya dakika ya 73 baada ya shuti kali la Jonjo Shelvey kumbabatiza na kujaa wavuni huku kipa De Gea akiwa hana la kufanya.
Van Gaal alimrejesha Rooney kwenye nafasi ya ushambuliaji akiungana na Robin van Persie huku Facao akisugua benchi lakini nahodha huyo wa United na England akapiga shuti moja tu lililolenga goli.
Kiwango cha Van Persie kilikuwa duni huku Angel di Maria, Marouane Fellaini na Daley Blind wakishindwa kuing'arisha timu vile ipasavyo.
Swansea (4-3-3): Fabianski 6.5; Naughton 6, Fernandez 7, Williams 7, Taylor 7; Cork 7, Shelvey 7 (Amat 90), Ki 7.5; Sigurdsson 6 (Montero 74, 6), Gomis 6, Routledge 6.
Manchester United: De Gea 6; McNair 5 (Valencia 46), Jones 6, Rojo 6, Shaw 5 (Young 59, 6); Blind 6; Herrera 6.5, Fellaini 5.5, Di Maria 6 (Mata 79), Rooney 6, Van Persie 5
Comments
Post a Comment