Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Luis Suarez amerejea kwenye ardhi ya England kwa kishindo baada ya kufunga magoli yote mawili ya Barcelona kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo mtamu wa Ligi ya Mabingwa.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa Etihad, Suarez alifunga katika dakika ya 16 na 30 na kuifanya Barcelona ipate faida ya magoli mawili ya ugenini.
City itakuwa na kibarua kigumu cha kushinda kwenye dimba la Camp Nou licha Aguero kupunguza bao moja dakika ya 69.
Gael Clichy akalimwa kadi nyekundu dakika ya 74 baada kuonyeshwa kadi njano kwa mara ya pili huku Lionel Messi akipoteza penalti dakika ya 90 baada ya kipa Joe Hart kupangua kwaju huo wa miguu 12.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Nasri (Fernandinho 61 mins), Milner, Fernando, Silva (Sagna 78), Dzeko (Bony 68), Aguero.
Barcelona: Ter Stegen, Alves (Adriano 75), Pique, Mascherano, Jordi Alba, Rakitic (Mathieu 71), Busquets, Iniesta, Messi, Suarez, Neymar (Pedro 80).
Comments
Post a Comment