Mchezo uliokuwatanisha wenyeji timu ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga dhidi ya timu ya Simba umeingiza jumla ya tsh. milioni 31.
Juma la watazamaji 5,439 waliingia uwanjani kushuhudia mchezo huo, ambao timu ya Stand imepata mgao wa tsh. 6,564,268.22 na Simba wakipata mgao wa tsh. 4,661,581.78.
VAT (18%) tshs. 4,763,135.59 huku FA mkoa wakipata tsh.665,940.25, FDF tsh. 1,141,611.86, Bodi ya Ligi tsh. 1,522,149.15, Gharama za mchezo tsh. 1,617,283.47, Uwanja tsh. 2,854,029.66, Gharama ya tiketi tsh. 1,593,000,00, FDF tsh. 2,921,000.00, TFF tsh.2,921,000.00
Katika uwanja wa Sokoine mbeya jumla ya tsh. 74,600.000.00, zilipatikana kutokana na watazamaji 14,920 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo, VAT(18%) tsh.11,379,661.02, CDRB (5%) tsh.3,730.000.00, FDF tsh. 5,222,000,00, TFF tsh. 2,238,000.00, Uwanja tsh. 7,804,550,85, Gharama za mchezo tsh 4,442,578.81, Bodi ya Ligi tsh. 4,162,427,12.
Chama cha soka mkoa (FA) Mbeya kimepata tsh. 1,821,061.86, FDF(TFF) tsh. 3,121,820.34, wenyeji timu ya Mbeya city wakipata tsh. 17,950,466.95 na klabu ya Yanga tsh. 12,747,438.98.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Comments
Post a Comment