Sokoine yawekwa chini ya ulinzi mkali



Sokoine yawekwa chini ya ulinzi mkali
DSC_0023-630x360
Na Amplifaya Amplifaya
SUALA la ushirikina limezidi kushika kasi kila kukicha katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara na hili lilidhihirika mapema mara baada ya mechi ya Prisos na Yanga siku ya Alhamis kukamilika ambapo wapenzi na mashabiki wa Mbeya City fc iliwabidi waingie uwanjani kulinda uwanja wao kuepusha ushirikina kwa kuhakikisha hakuna anayeingia uwanjani humo wala kukatiza.
Mashabiki hao hawakuwa na imani kabisa na kila mtu anayekatiza eneo hilo la uwanja na isitoshe iliwabidi watumie nguvu ikiwemo vichapo kwa wale wote walioenda kinyume na agizo lao, moja kati ya watu waliokutwa na mkasa huo ni shabiki maarufu wa Yanga anayepaka masizi usoni na kuweka tambara usoni anajulikana kwa jina la Ally Yanga.
Shuhuda aliyeshuhudia tukio hilo alisema mapema tu Mara baada ya mchezo kuisha na mahojiano kumalizika ya walimu wa timu zote tofauti, mashabiki waliingia na kusema amri ya kutoingia kwenye pitch au kukatiza uwanjani kwa imani ya kufanyiwa uchawi.
"Tupo hapa kwaajili ya kulinda uwanja wetu usidhurike iwe kwa njia za kichawi au njia tofauti, hatutaki timu yetu ipoteze kama Prisons walivyopoteza" alisema shabiki huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe hadharani.
Kumbuka Yanga haijawahi kuifunga Mbeya City katika uwanja wa Sokoine tangu timu hiyo ipande ligi kuu na hii itakuwa Mara ya pili wanakutana katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.


Comments