Siri ya Simba kufa Shinyanga yaanikwa



SAM_4586

"Siri ya ushindi ni kukaa na wachezaji wangu mara kwa mara, nawasisitiza kupambana kusaka ushindi, ligi imekuwa ngumu, hatuko nafasi nzuri, nafurahi mechi dhidi ya Simba wameonesha kiwango kizuri"

"Simba ni klabu kubwa, mafanikio yao ni makubwa, lakini tulijipanga vizuri hasa baada ya kushinda mechi iliyopita 4-1 na Mgambo JKT"

"Haikuwa kazi rahisi, tumepata kadi mbili za njano, tutamkosa Ubwa (Abuu) na Mustapha (Yassin) katika mechi yetu nyingine ya nyumbani na Kagera Sugar (februari 28 mwaka huu). Kagera ni wenzetu, wanatumia uwanja wa kwetu, najua itakuwa mechi ngumu, lakini nina wachezaji wengi wa kuziba nafasi ya wale watakaokosekana"

Hayo yalikuwa maneno ya kocha wa Stand United, Mganda, Mathias Lule, baada ya kuifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Bao pekee la ushindi wa Stand United lilifungwa na Mnigeria, Abasirim Chidiebele.

Kwa matokeo ya jana, Stand wamepanda mpaka nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu wakijikusanyia pointi 18 baada ya kushuka dimbani mara 16.



Comments