Simba yampiga chini kiongozi mmoja mwandamizi




Simba yampiga chini kiongozi mmoja mwandamizi
Kikosi cha Simba
UONGOZI wa Simba Sports Club ya jijini Dar es salaam umempiga 'stop' au kumzuia mmoja kati ya viongozi kufika kambini kwao ka maslahi ya timu.
 
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa timu zinasema kuwa tayari kiongozi huyo mwandamizi ameshazuiliwa na taarifa ameshazipata.
 
" Kweli kuna hatua zimechukuliwa na uongozi na tumeona kila anapokwenda linakuwa tatizo kubwa mno, amekuwa akichangia kuwavuruga wachezaji na tulichoamua ni kwamba, asiende kwenye kambi ya timu itakapokuwa nje ya mkoa au Dar es salaam.
 
" Mara kadhaa tumepata malalamiko kutoka kwa wachezaji wamekuwa wakilaumu sana kwamba anawachanganya na pia anawapa maneno ya kashifa kitu kinachowavunja nguvu.
 
"Wachezaji pia wamelalamika kuwa amekuwa akiwapiga vita kwa kumwambia kocha kuwa hawafai lakini wanapokutana naye anawachekea"
 
Hivi karibuni pia kocha wa timu hiyo Goran Kopunovic alifunguka na kusema kuna kiongozi ambaye amekuwa akimpangia kikiso cha timu na baadayee mwenyekiti wa kamati ya usajili, bwana  Zacharia Hans Poppe alikataa ushauri wa kiongozi huyo na haikuwa kulazimisha bali ni ushauri tu.


Comments