Simba wavunja rekodi ya mechi za ugenini Shinyanga



Simba wavunja rekodi ya mechi za ugenini Shinyanga
SAM_4578
Chidiebeze ndiye muuaji wa Simba Shinyanga
BAO pekee la Mnigeria, Abasirim Chidiebeze limetosha kuipa Stand United  ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyopigwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Stand walimaliza mechi wakiwa wachezaji 9 uwanjani baada ya Yassin Mustapha na Abuu Ubwa Zuberi kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Mashabiki wa Stand United walifurika
Simba ikicheza chini ya vigogo wake walioongozwa na Rais Evans Aveva na mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hans Poppe walishindwa kabisa kuonesha cheche zao.
Kwa matokeo hayo, Simba wanaendelea kushika nafasi nne kwa pointi zao 20 baada ya kushuka dimbani mara 15.
Stand United wamepanda kutoka nafasi ya 12 mpaka 10 wakijikusanyia pointi 18 baada ya kushuka dimbani mara 16.
Simba wamepoteza mechi ya kwanza ugenini Msimu huu. Wamecheza mechi 8 ugenini, wameshinda 2, wamepoteza 1 na wametoka sare 5.


Comments