Simba Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu


Simba Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu

Na Amplifaya Amplifaya

avevaaSiku zote unapokuwa puppet au kibaraka kwa lugha ya kiswahili mbali na hilo au kuwa mbabe katika uongozi hakutakuwa na tija hata kidogo na hakutakuwa na matokeo mazuri.

Kingine ni hili suala la matabaka katika sehemu ambayo umoja unahitajika ili kujenga kitu cha msingi ambao utasimama bila kuwa na nyufa ni kama tu unapoanza kujenga nyumba yako mtu wangu, usipotengeneza vizuri msingi wa jambo utaishia kuona nyumba inadondoka au nyufa zinaanza kutokea.

Haya ni mambo mawili ambayo Simba imekumbwa nayo kwa wakati huu na chanzo kikubwa ni uongozi uliopo madarakani bila kupepesa macho.

Matabaka yameiandama Simba toka kwa Uongozi wenyewe hadi kwa wachezaji wenyewe wanakuwa na matabaka.

Ninapoongelea wachezaji nabase moja kwa moja kutokana na jinsi value zao na jinsi wanavyokuwa treated bila usawa. Utakuta yule anapata kila kitu na mwingine hapati kiufupi tu lazima wachezaji hawatakuwa na morality nzuri katika kucheza mpira.

Baadhi ya viongozi au Kiongozi kuzuiwa kuingia katika kambi ya timu lazima pande moja itakuja na mtazamo tofauti na kwa situation hiyo hakuna umoja utakaokuwepo.

Simba kama Brand hakuna haja ya kuwa na matabaka au kutotimiza mahitaji kwa wachezaji hakuna la maana ambalo litafanyika watu wangu.

Nawapongeza Yanga kwasasa walio na umoja na wapo kwenye morality nzuri hivi sasa na imekuwa timu ya kuigwa na haya Simba iwe mfano wa kuiga jinsi Yanga wanavyofanya hivi sasa hakuna kabisa matabaka.

Ni halali yako kushare mawazo yako mtu wangu au kama una breaking News kuhusiana na matukio ya kimichezo au maoni au hata ushauri unaolenga kufika sehemu husika, tuma na tutafikisha sehemu husika mawaidha yako kwa njia ya WhatsApp +255688665508.



Comments