Simba ilivyo iangamiza Prisons bila huruma


Simba ilivyo iangamiza Prisons bila huruma

IMG_6097Na. Richard Bakana, Dar es salaam

Baada ya kuanza kwa sare nyingi katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania bara, klabu ya Simba leo imefanikiwa kuwatoa majonzi mashabiki wake kwa kuifunga Tanzaia Prisons kwa jumla ya maba 5-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

Dakika ya 1 Simba wanapata faulo inayopigwa na Eamanuel Okwi baada ya kufanyiwa madhambi lakini inakuwa mboga ya Kipa wa Prisons Ahmed Yusuf.

Prisons wanafanikiwa kupeana pasi vyema hadi katika eneo la 18 la Simba lakini pasi ya Mwisho inakuw haina macho kwaninKipa wa Simba Ivo Mapunda anainyaka na kuanza upya mashambulizi.

Ramadhan Singano katika dakika ya 10 anapiga krosi safi inayomkuta Okwi lakini anashindw kufanya kitu baada ya kubanwa na mabeki wa Tanzania Prisons.

Dakika ya 12 Dan Serunkuma anapiga kicha zohofu baada ya kupokea krosi ya Jonas Mkude ambapo mpira unamgonga kichwa ni na kutoka nje.

Ibrahim Ajib anaipatia Simba bao la kwanza katika dakika ya 15 kufatia kazi nzuri ya Dan Sernkuma ambaye anawazidi nguvu mabeki wa Prisons na kumpitishia Ajibu pasi ya chini na kuutumbukiza mpira langoni.

Dakika ya 18 Simba wanapata kona ya kwanza baada ya Ibrahim Ajibu kuambaa na mpira akiwa ndani ya 18 ambapo mabeki wa Prisons wanapokonya mpira na kuutoa nje.

Kwa mara ya pili Ibrahim Ajib anaandika bao la pili dakika ya 21 baada ya kipa wa Prisons Ahmed Yusuf kushindwa kudaka mpira na kuutema ambapo unamkuta mshambuliaji huyo na kumpiga chenga kipa na kuandika bao, yote ni baada ya Okwi kupiga shuti kali ambalo kipa anathema.

Simba wanapata kona ya pili inayopigwa na Ramadhan Singano katika dakika ya 24 lakini kipa Ahmed Yusuf anaipangua na kurudi ndani zaidi.

Dakika  ya 28 Okwi anamtazama Dani Serunkuma ambapo anampigia krosi safi lakini Mganda huyo anashindwa kuiandikia samba bao la tatu.

Dakika ya 30 Dan Serunkuma anaiandikia Simba bao lakini muamuzi anakataa akidai alikuwa ameibia, hiyo ilikuwa baada ya Emanuel Okwi kupiga shuti kali ambalo linamshinda kipa Ahmed Yusuf na kumkuta Serunkuma.

Tanzania Prisons wanakosa bao kupitia kwa Bonface ambaye alikuwa anaenda kukutana na Ivo Mapunda lakini akasita na mpira kuokolewa na mabeki wa Simba dakika ya 33.

Dakika ya 34 Mtibwa wanamuingiza Jonh Matei na kumtoa Elfadhil.

Dakika 38 Dan Serunkuma anfanya kazi kubwa ya kuwatoka mabeki wa Prisons lakini anapitisha pasi safi ambayo washambuliaji wa Simba wanajikanyaga na kushindwa kupachika bao.

Simba wanapata Penati dakika ya 41 baada ya Okwi kuingia na mpira katika 18 ya Prisons ambapo anaurudisha nyuma na kupigwa ambapo unamgonga Mwagama mkononi na kuwa Penati.

Dakika ya 42 Ibrahim Ajib anaiandikia timu yake bao la 3 kwake na timu yake pia kufatia kupiga penati hiyo.

Hadi dakiak ya 45 mwamuzi Adam Odongo anapuliza kipenga cha mwisho Simba ilikuwa inaongoza kwa bao 3-0.

Simba wakianza kipindi cha pili kwa kasi kubwa, kunako dakika ya 46 Jonas Mkude aliikosea bao timu yake baada ya kupiga shuti akiwa ndani ya 18 na kupaa juu.

Dakika ya 47 David Mwamaja anaamua kumuingiza Julius Kwanga na kumtoa Boniface Hau, adamu Chimbongwe pia anatolewa na Meshack Said anaingia kusaidia kutafuta japo bao la kufutia machozi.

Prisons katika dakika ya 52 wanakosa bao kupitia kwa Julius Kwanga baada ya kubaki na kipa lakini anapiga mpira unaotoka juu ikiwa ni baada ya kuzongwa na mabeki wa Simba wakiongozwa na Joseph Owino.

Emaniel Okwi katika dakika ya 59 anawakimbia mabeki wa Prisons na kuingia ndani ya 18 ambapo anapigiga krosi, Dan Serunkuma anajaribu kupiga tikitaka lakini anaukosa na kumkuta Ramadhan Singano anapiga shuti na kupaa nje ya lango la Tanzania Prisons.

Dakika ya 61 Ibrahim Ajib anapewa kadi ya Njano baada ya kutaka kufunga bao kwa mkono.

Dakika ya 65 mshambuliaji wa Prisons  Kwanga anakosa kuipatia timu yake bao

Kocha Kopunovich anaamua kumpumzisha Ibrahi Ajib katika dakika ya 66 na nafasi yake anaingia Hawadhi Juma.

Nurdin Chona wa Prisons anatolewa nje kwa kadi Nyukundi kufatia kuwa na kadi ya kwanza ya njano baada ya kumfanyia madhambi Ramadhani Singano kunako dakika ya 67.

Dakika ya 72 Said Ndemla anapiga shuti kali nje ya 18 ya Prisons lakini inatoka nje.

Emanuel Okwi anaifungia Simba bao la 4  baada ya kuwminya mabeki wa Prisons na kupiga mpira ambao unamuacha kipa akiwa hana cha kufanya kunako dakika ya 74.

Dan Serunkuma anapumzishwa katika dakika ya 76 na nafasi yake kuchukuliwa na Twaha.

Ramadhan Singano anaifungia Simba bao la tano katika dakika ya 82 baada ya kazi safi ya Emanuel Okwi na kuwaacha mabeki wa Prisons wakiwa hawana kitu cha kufanya.

Dakika ya 90 Simba wanakosa bao kupitia kwa Hawadhi baada ya kupiga shuti kali ambalo linapanguliwa na kipa wa Prisons na kuwa kona.

Hadi dakika ya 90 za mchezo huo zinamalizika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Simba wanakuwa wametoa zawadi nzuri kwa mashabiki wao kuelekea mkutano hapo kesho kwa ushindi wa bao 5-0 dhidi ya Tanzania Prisons.



Comments