‘Saimon Msuva, mpishi na kinara wa mabao Yanga SC, huu ndiyo moto wake…’


'Saimon Msuva, mpishi na kinara wa mabao Yanga SC, huu ndiyo moto wake…'

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,

Novemba, 2012 niliwahi kuandika makala kuhusu kiungo-mshambulizi, Saimon Msuva. Makala ambayo nilielezea namna mchezaji huyo anavyoweza kujiimarisha na kuwa mchezaji bora nchini. Msuva ndiyo kwanza alikuwa na miaka 19, alipangwa na aliyekuwa kocha wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen katika kikosi cha kwanza cha Stars katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Burundi katika michuano ya CECAFA Challenge Cup nchini Uganda.

Licha ya kuichezea Yanga SC kwa miezi miwili akitokea Moro United, mchezaji huyo alionesha ' wasiwasi' na hali ya kutojiamini katika mchezo wake wa kwanza akiwa mchezaji wa timu ya Taifa. Kim alimuanzisha katika wing ya kulia lakini hakuna ambacho aliweza kufanya na wakati Mbwana Samatta na Tomas Ulimwengu walipojumuika na timu, Msuva akarudishwa benchi na hakupata tena nafasi katika kikosi cha kwanza cha Stars ambacho kilimaliza katika nafasi ya nne katika michuano ile.

msuva
Sikuvutiwa na uchezaji wa kuinama chini ambao Msuva aliuonesha katika mchezo huo ambao Stars ilichapwa bao 1-0 na Burundi lakini niliamini kama mchezaji huyo ataendelea kutumika katika klabu yake angeweza kujirekebisha na kuwa mchezaji tishio.

ERNIE BRANDTS, ambaye alichukua nafasi ya Tom Saintfiet, Septemba, 2012 kama mkufunzi mkuu wa Yanga aliweza kumfanya mchezaji huyo kujiamini; pia akimsaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza tatizo la kutazama chini. Mashabiki baadhi klabuni kwake Yanga walikuwa wakimzomea mchezaji huyo lakini mara baada ya timu kurejea kutoka katika kambi ya wiki mbili nchini Uturuki, Msuva akawa ' mchezaji wa mashabiki'.

Alionekana kuwasaulisha mashabiki wa timu hiyo kuhusu kiungo-mshambulizi, Mrisho Ngassa ambaye alikuwa nje ya timu hiyo kwa misimu mitatu mfululizo. Ngassa ' wing bora zaidi wa upande wa kulia' nchini aliwateka mashabiki wa Yanga kwa misimu mitatu mfululizo ( 2007-2010) alipojiunga na Azam FC, lakini kitendo cha Msuva kutengeneza magoli mengi ya Yanga katika michezo ya mzunguko wa pili msimu wa 2012/13 na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa 24 wa ligi kuu Tanzania Bara kilifanya mashabiki wengi kumuamini mchezaji huyo.

Msuva alikuwa alitokea kuwa mpiga krosi mahiri, wing hasa wa pembeni ambaye muda wote hukimbia pembeni mwa uwanja kutafuta nafasi. Licha ya kiwango cha juu katika kasi, wepesi, umakini katika utoaji wa pasi mchezaji huyo bado alikabiliwa na tatizo la kushindwa kucheza katika nafasi nyingine uwanjani zaidi ya ' namba7′.

msuva 1

BILA SHAKA ALIKUWA MCHEZAJI BORA WA MSIMU YANGA SC, 2013/14,

Utawala wa Yanga ulifanya jitihada kubwa kuhakikisha ' mchezaji wa klabu', Ngassa anarejea katika timu hiyo. Inawezekana ni mapenzi binafsi kati ya Yanga na Ngassa ndiyo yaliyopelekea pande hizo kufanya kazi kwa mara nyingine, lakini kimpira usajili wa Ngassa katikati ya mwaka 2013 haukuwa na sababu muhimu. Brandts tayari alikuwa na timu bora ya muda mrefu, Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kizza, Athumani Iddi ' Chuji' na Haruna Niyonzima ndiyo walikuwa muhimili wa timu msimu ambao walitwaa ubingwa huku wakiishinda Simba SC kwa magoli 2-0, Mei, 2013.

Ngassa alifungiwa takribani michezo saba hivyo alitakiwa kukosa michezo sita ya mwanzo katika ligi kuu msimu wa 2013/14 na mchezo wa Ngao ya Jamii. Msuva akapewa nafasi ya kuendelea kucheza katika kikosi cha kwanza, licha ya kutengeneza magoli matano katika michezo sita ya mwanzo, Saimon akarudishwa benchi katika mchezo wa saba dhidi ya mahasimu wao Simba na Ngassa akaanza sambamba na Kavumbagu na Kizza katika safu ya mashambulizi. Yanga ilikuwa mbele kwa magoli 3-0 hadi nusu ya kwanza ya mchezo inamalizika, na timu ilionekana kucheza vizuri na kasi katika mfumo wa 4-3-3.

Kiwango cha Ngassa katika mchezo ule kilizima kabisa matumaini ya Msuva kusudi katika kikosi cha kwanza. Ngassa alifunga mabao sit katika michezo yake saba ya mwanzo katika ligi kuu wakati Msuva alfunga mabao matano kwa msimu mzima. Kuondolewa kwa Brandts ilikuwa ni jambo jema kwa Msuva kwani mwalmu aliyefuata, Hans Van Der Plujm alimrudisha mchezaj huyo katka kikosi cha kwanza mwanzoni mwa mwaka 2014. Ni nani alimpisha Msuva katika kikosi cha kwanza?

Ngassa, Kavumbagu, Emmanuel Okwi ikasa safu ya mashambulizi, wakati Msuva akibeba majukumu ya Niyonzima kama kiungo mchezesha timu na mpkaj wa mabao. Kitendo cha kuanza kuchezeshwa kama kiungo wa kulia au akitokea katikati ya uwanja kilimfungilia nafaai nyngi za kufunga mabao. Akitumia kasi yake, Msuva ana uwezo wa kupiga mashut hata akiwa katika ' spidi', hujbadilisha na kujivika ' tabia za mshambuliaji pale anapokuwa ndani ya eneo la hatari'.

Hata kama Yanga iliutema ubingwa mbele ya Azam FC, Msuva alivutia kila mmoja kutokana kiwango chake . Kwangu alikuwa mchezaji bora wa klabu kwa kuwa alijituma zaidi kutetea nafasi yake katika kikosi cha kwanza na kufanikiwa licha ya kuwa na umri mdogo. Alikubali kushindania nafasi na hakuhofia majina makubwa katika kikosi. Hakika alifanikiwa.

2014/2015………
Tayari amefunga mabao 25 tangu alipojiunga na Yanga katikati ya mwaka 2012, huku akiwa kinara wa mabao kwa klabu yake msimu huu, Msuva ni mchezaji wa ' hatari zaidi' katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu, kasi yake namsaidia kufika katika maeneo muhimu katika muda mwafaka, ni mchezaji makini sana. Amefunga magoli saba katika ligi kuu msimu huu, amefunga mabao manne katika michezo minne ya Mapindu Cup, Januari mwaka huu huko Visiwani Zanzibar, pia alifunga moja ya mabao matatu katika ushndi wa 3-0 dhidi ya Azamfc ambao Yanga waliupata katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Septemba, 2014.

Ukichanganya mabao hayo utaagundua kuwa mchezaji huyo amefunga mabao 12 katika mashindano yote msmu huu, huku akishirIki katika upigaji wa pasi nyngi zilizozaa mabao. Hans alimfanya kucheza sambamba na Ngassa na sasa amemuondoa Mliberia, Kpah Sherman katika kikosi cha kwanza na kuwapanga kwa pamoja, Ngassa, Andrey Coutinho na Msuva ambao humzunguka Amis Tambwe na mbinu hiyo imekuwa na mafanikio makubwa .

Ngassa alifunga mabao yote mawili katika ushindi wa Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar kisha Tambwe kufunga mara mbili katika mchezo uliofuata dhidi ya BDF IX katika Michuano ya Shirikisho Afrika, Msuva akafunga mara mbili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons kabla ya watatu hao kila mmoja kufunga mara moja katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Mbeya City FC.

0714 08 43 08



Comments