Uhusiano mbovu wa Roy Keane na Sir Alex Ferguson hauna dalili ya kumalizika mara baada ya 'mahasimu' hao wawili kuchuniana kwenye ndege wakati wakirejea nyumbani Manchester Jumatano mchana wakitokea Paris, Ufaransa.
Kocha huyo wa zamani wa Manchester United na nahodha wake wa zamani, walisafiri katika ndege moja AF1068 iliyoondoka kwenye uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle airport saa 7 kasoro dakika 5, lakini kila mmoja akapuuzia kutambua uwepo wa mwenzake katika muda wote wa safari iliyochukua saa nzima.
Keane na Ferguson wote walikuwa Ufaransa kuangalia mechi ya Ligi ya Mabingwa Jumanne usiku kati ya Paris Saint-Germain na Chelsea iliyomalizika kwa sare ya 1-1.
Comments
Post a Comment