Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amewatoa shaka wote wanaoshuku uwezo wake baada ya kuifungia Real Madrid bao moja na kutengeneza lingine katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Schalke 04 kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Ronaldo alifunga kwa kichwa dakika ya 25 akimalizia krosi tamu ya Carvajal kabla hajamtengenezea beki Marcelo aliyefunga bao la pili dakika ya 78.
Kwa ushindi huo wa ugenini, Real Madrid imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali. Katika mchezo mwingine Basel na FC Porto zilitoka sare ya 1-1.
Schalke: Wellenreuther, Uchida, Howedes, Matip, Nastasic, Aogo, Neustadter (Kirchoff 56'), Hoger (Meye 81'), Boateng, Choupo-Moting, Huntelaar (Platte 32')
Real Madrid: Casillas, Marcelo, Pepe, Varane, Carvajal (Arbeloa 81'), Silva, Kroos, Isco (Illarramendi 84'), Bale, Benzema (Hernandez 78'), Ronaldo.
Comments
Post a Comment